• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yataka kuanzisha tena mazungumzo na kundi la Taliban

    (GMT+08:00) 2019-09-09 20:16:10

    Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo amesema, mazungumzo kati ya Marekani na kundi la Taliban yanaonekana kusimama kwa sasa, lakini nchi hiyo inataka kuanzisha tena mazungumzo hayo katika siku za baadaye.

    Bw. Pompeo amesema Marekani imemrejesha mjumbe maalumu wa nchi hiyo anayeshughulikia mambo ya makubaliano ya amani ya Afghanistan Bw. Zalmay Khalilzad, ili kuweka mpango wa hatua katika kipindi kijacho.

    Ameongeza kuwa kuanzisha tena mazungumzo hayo kunategemea kundi la Taliban. Kundi hilo linatakiwa kuthibitisha kwa Marekani kuwa linaweza kutimiza matakwa yaliyotolewa na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako