• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia na Ufaransa zaendelea kushirikiana kudumisha makubaliano ya suala la nyuklia la Iran

    (GMT+08:00) 2019-09-10 08:48:58

    Waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergei Lavrov amesema, Russia na Ufaransa zitaendelea kushirikiana kudumisha makubaliano ya nyuklia ya Iran (JCPOA) kwa ukamilifu.

    Baada ya mkutano kati ya mawaziri wa mambo ya nje na ya ulinzi wa Russia na Ufaransa, Bw. Lavrov amesema, pande hizo mbili zimekubaliana kwamba hakuna njia nyingine ya kutatua suala la Iran. Kuhusu Russia na Ukraine kubadilishana wafungwa hivi karibuni, Bw. Lavrov amsema Russia inatumai kuwa hatua hiyo ni ishara njema ya kutatua suala la eneo la Donbass mashariki mwa Ukraine na kutarajia kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili unaweza kurejea kwenye hali ya kawaida.

    Kwa upande wake, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Bw. Jean-Yves Le Drian amesema, Ufaransa inatarajia mkutano wa Normandy Four utakaolenga kutatua mgogoro wa Ukraine utaweza kufanyika hivi karibuni, mjini Paris. Ufaransa inaona ni lazima kusukuma mbele utekelezaji wa makubaliano ya Minsk chini ya mazingira mazuri ya sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako