• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Kikao cha mageuzi ya ligi ya mabingwa Ulaya chaanza jana kinatarajiwa kukamiliza leo

    (GMT+08:00) 2019-09-10 09:22:44
    Chama cha klabu za Ulaya (ECA) kimeanza mkutano wake wa siku mbili jijini Geneva Uswisi huku uongozi ukikabiliwa na mgomo wa wanachama wake. ECA inaongozwa na mwenyekiti wa klabu ya Juventus, Andrea Agnelli inahusishwa kwa karibu kupata mapendekezo ya kufanya magezusi mashindano hayo makubwa ya klabu kuanzia mwaka 2024.

    Mapendekezo hayo yaliwasilishwa na chama cha soka Ulaya (UEFA) mwezi Mei, mageuzi hayo yanajumuisha kuanzishwa kwa mechi za mwishoni mwa wiki, makundi manne ya timu nane, mfumo wa mpangilio wa kushuka na kupanda amabo utahakikisha timu sita za juu kutoka kila kundi zinafuzu moja kwa moja kucheza michuano ya msimu unaofuata.

    Mwezi uliopita UEFA ilitangaza kufuta kikao na ECA na ligi za Ulaya, chombo kikubwa zaidi kinachowakilisha zaidi ya klabu 900 kilichopangwa kufanyika Septemba 11.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako