• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Cameroon na Tunisia kuimarisha ushirikiano kwenye kuendeleza miundo mbinu

    (GMT+08:00) 2019-09-10 19:33:50

    Cameroon na Tunisia zimekubaliana kuimarisha mawasiliano na kubadilishana uzoefu na kuchangia fursa za kuhimiza maendeleo ya miundo mbinu kwenye nchi hizo mbili.

    Waziri wa zana, ujenzi na mipango miji wa Tunisia Bw. Nourreddine Selmi amewaambia wanahabari baada ya kukutana na waziri mkuu wa Cameroon Bw. Joseph Dion Ngute kuwa Tunisia una uzoefu mkubwa kwenye ujenzi wa nyumba.

    Waziri wa nyuma na mipango miji wa Cameroon Bibi Celestine Ketcha Courtes, amesema uzoefu wa Tunisia  kwenye ujenzi wa nyumba ni muhimu kwa Cameroon, ambayo inahitaji kuwa nchi inayoibuka kabla ya mwaka 2035.

    Amesema wanataka kuanzisha ushirikiano wenye nguvu ili kuunga mkono ujenzi wa nyumba za bei nafuu, barabara na miundo mbinu mingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako