• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Uingereza lakataa tena pendekezo la waziri mkuu la kufanya uchaguzi mkuu mapema

    (GMT+08:00) 2019-09-10 20:03:34

    Baraza la chini la Bunge la Uingereza limekataa tena pendekezo la kufanyika kwa uchaguzi mkuu mapema Oktoba 15 lililotolewa na waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Boris Johnson. Baada ya hapo, bunge hilo limeanza rasmi mapumziko ya wiki tano.

    Bw. Johnson usiku wa tarehe 4 aliwahi kutoa pendekezo la kufanyika uchaguzi mkuu mapema baada ya baraza la chini la bunge hilo kupitisha mswada unaolenga kuizuia Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya bila makubaliano, lakini pendekezo hilo lilishindwa kupitishwa.

    Baada ya kutolewa kwa matokeo ya upigaji kura, Bw. Johnson amesema serikali itaendelea kufanya juhudi kufikia makubaliano na Umoja wa Ulaya wakati wa mapumziko ya bunge hilo, huku ikifanya maandalizi ya kujitoa Umoja huo bila makubaliano.

    Bw. Johnson amesisitiza kuwa kamwe hatautaka Umoja wa Ulaya kuahirisha nchi hiyo kujitoa Umoja huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako