• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa tatu wa mambo ya usafirishaji wa vifurushi ya dunia wafanyika China

  (GMT+08:00) 2019-09-11 19:16:43

  Mkutano wa tatu wa mambo ya kupeleka vifurushi ya dunia wenye kauli mbiu ya "Vifurushi vinaiunganisha dunia" umefanyika jana mkoani Zhejiang, mashariki mwa China. Washiriki zaidi ya 600 kutoka sekta mbalimbali wamehudhuria mkutano huo, wakijadili namna ya kuharakisha mambo ya kusafirisha vifurushi ya China yaende nje.

  Mkuu wa Idara ya posta ya China Bw. Ma Junsheng ametoa hotuba akisema mambo ya usafirishaji wa vifurushi nchini China yanaendelea vizuri, na idadi ya vifurushi vitakavyosafirishwa mwaka huu inatarajiwa kufikia zaidi ya bilioni 60. Hata hivyo, idadi ya vifurushi vinavyosafirishwa kwenda nje ya nchi kwa mwaka ni takriban bilioni 2, kiasi ambacho kinachukua asilimia 3 tu ya kiasi cha jumla kwa mwaka.

  Ameongeza kuwa China inapaswa kuharakisha hatua yake ya kwenda nje kwenye sekta ya kutuma vifurushi, ikiwa ni pamoja na kupanua mtandao wa huduma, kuzidisha ushirikiano kati ya sekta tofauti, kuhimiza uvumbuzi wa kiteknolojia, na kuboresha mazingira ya biashara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako