• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Zaidi ya 10,000 bado hazijachukuliwa

  (GMT+08:00) 2019-09-11 19:42:32
  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Kilimanjaro, imesema kuna zaidi ya leseni 10,000 za madereva wa magari ambazo zimekamilika, lakini wahusika wamezitelekeza bila kuzichukua kwa muda mrefu sasa.

  Meneja wa TRA mkoani wa Kilimanjaro, Gabriel Mwangosi, amesema kuwa ziko leseni ambazo zilitelekezwa au kuachwa kwa muda mrefu hadi muda wake wa matumizi kwisha na maofisa wake kulazimika kuziteketeza kwa kuzichoma moto.

  Mwangosi alisema hayo baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anna Mghwira, kwenda kukagua shughuli zinaziofanywa na maofisa wa TRA na kuzungumza nao kuhusu mambo mbalimbali.

  Kwa nyakati tofauti, baadhi ya watu wanaoomba leseni katika mamlaka hiyo, wamekuwa wakilalamikia kucheleweshwa kwa leseni hizo wakidai kwamba wanaambiwa hakuna karatasi ngumu za kutoa leseni hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako