• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vya nchi za magharibi vyalaaniwa na Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2019-09-12 17:46:17

    Mkutano wa 42 wa Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa umefanyika tarehe 10 hadi 11 mwezi huu, ambapo mashirika mengi yasiyo ya kiserikali yamelaani vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vya baadhi ya nchi za magharibi kwenye mdahalo uliofanyika kwenye mkutano huo.

    Baraza la amani ya dunia limesema kitendo cha Marekani kuingilia mambo ya ndani ya nchi za Latin Amerika kama Venezuela, kimekiuka Katiba ya Umoja wa Mataifa, na kukiuka haki ya kujiamulia mambo na mamlaka ya nchi.

    Kituo cha utafiti wa vijana kimelaani hatua za Marekani za upande mmoja dhidi ya Venezuela, ikiwa ni pamoja na kuweka vikwazo vya kiuchumi, kuzuia mali za serikali ya Venezuela nchini Marekani, na kuweka marufuku ya kuuza nje mafuta ya Venezuela.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako