• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ghana yazindua kampeni ya chanjo dhidi ya polio

  (GMT+08:00) 2019-09-12 19:41:23

  Mamlaka za afya nchini Ghana zimezindua kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Polio. Kampeni hiyo inafanyika kwa muda wa siku nne katika mji mkuu na maeneo ya karibu ya mji huo, ambapo maofisa wa afya na watu wanaojitolea, watakwenda nyumba hadi nyumba, watamtembelea masoko, vituo vya magari na sehemu nyingine ili kutoa chanjo kwa watoto.

  Ghana haijakumbwa na maambukizi ya ugonjwa wa polio tangu mwaka 2009, kabla ya maambukizi ya watoto watatu kuripotiwa mwezi Julai mwaka huu. Mkuu wa Idara ya huduma za afya ya Ghana Bw. Anthony Nsiah Asare, amewahimiza wazazi na wanaotunza watoto, kuhakikisha kuwa watoto wao wanapatiwa chanjo katika kipindi hicho.

  Kazi ya ufuatiliaji kuhusu chanjo hiyo mjini Accra itafanyika baadaaye mwezi huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako