Katika ujumbe uliowekwa kwenye akaunti ya Twitter ya CBK, benki hiyo ilikariri kuwa baada ya tarehe hiyo, noti zote za zamani hazitatumika tena.
Aidha katika ujumbe huo kwenye mtandao wa Twitter,CBK imetoa wito kwa wakenya kuwakumbusha wazee wanaoishi vijijini kubadilisha pesa za zamani kabla makataa.
Inaaminika kuwa watu wazima katika jamii za Kiafrika hupenda kuhifadhi pesa katika nyumba zao. Hii ndio maana asasi hii ambayo husimamia sekta ya benki imetoa wito huu.
Wakati huohuo CBK imekuwa ikitoa wito huo kila siku kupitia matangazo yaliyolipiwa katika magazeti ya kila siku yanayochapishwa humu nchini, redio na runinga.
Katika jumbe hizo umma hukumbushwa kuhusu siku ambazo zimesalia kabla ya muda wa matakataa uliowekwa kutamatika.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |