• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yafaidika pakubwa na uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI)

    (GMT+08:00) 2019-09-12 19:53:23

    Ethiopia imezipiku nchi za Afrika Mashariki mwaka jana kama mpokeaji mkuu wa uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni (FDI).

    Haya ni kulingana na Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la EY.

    Ripoti ya Utafiti wa Kuvutia wa EY wa mwaka 2019 iliyotolewa wiki hii inaonyesha kuwa Ethiopia ilivutia uwekezaji wa kigeni wa gharama ya Shs26.8 trilioni mwaka jana.

    Kenya ilifuata kwa karibu Shs7.68 trilioni huku Tanzania ikivutia uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni wa Shs3.8 katika kipindi sawa na hicho.

    Kulingana na Ripoti hiyo ya EY,nchini Ethiopia,uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni wa Shs26.8 trillion ulisababisha uzalishaji wa ajira 16,000 kutoka miradi 29 huku ajira 6,000 zilizalishwa Kenya kutokana na miradi 64.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako