• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: SOKA: Vita vya kugombea kiatu cha dhahabu EPL

  (GMT+08:00) 2019-09-13 07:54:42
  Baada ya mechi nne za ligi kuu ya Uingereza (EPL), tayari vita ya kuwania tuzo ya ufungaji bora ya kiatu cha dhahabu imeanza kushika kasi mapema.

  Katika usajili wa safari hii, timu nyingi za EPL ziliwekeza katika kupata wafungaji wazuri wa kuwafungia mabao mengi. Dalili zinaonekana kutakuwa na vita kali ya kuwania tuzo ya mfungaji wa bora wa ligi kwa msimu huu wa 2019/20.

  Zamani tuzo hii ilikuwa inashindaniwa zaidi na washambuliaji wa kati lakini katika miaka ya karibuni kuna mawinga wameonyesha ukali katika kufunga.

  Msimu uliopita kulikuwa na ushindani mkubwa wa kuwania ufungaji bora, ambapo mastaa watatu walifungamana, Mohamed Salah na Sadio Mane wa Liverpool na Pierre- Emerick Aubameyang wa Arsenal, ambao wote walipachika mabao 22 kila mmoja. Kuna uwezekano mkubwa hali hiyo ikajitokeza tena katika msimu huu wa 2019/20.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako