• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Tanzania amteua kiongozi mpya wa ujasusi

  (GMT+08:00) 2019-09-13 08:25:09
  Rais John Magufuli jana alimteua Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa ya Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Kamishna Diwani Athuman Msuya ameteuliwa na rais Magufuli kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, na mkurugenzi wa sasa Modestus Kipilimba atapangiwa kazi nyingine. Kabla ya kuteuliwa kwake, Kamishna Msuya alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako