• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wadau wa viwanda na biashara wa Hongkong watoa wito wa kutumia vizuri fursa ya kujiunga na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

    (GMT+08:00) 2019-09-13 17:22:28

    Shirikisho kuu la vyama vya wafanyabiashara vya China la Hongkong jana liliandaa tafrija, likitafiti umaalumu wa kipekee wa Hongkong kujiunga na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Washiriki kutoka sekta ya viwanda na biashara wanaona pendekezo hilo limetoa fursa kubwa kwa Hongkong, na Hongkong inatakiwa kuonesha vya kutosha sifa yake katika kukusanya fedha na utoaji wa huduma bora, kujiunga na pendekezo hilo ili kupata maendeleo kwa pamoja na taifa.

    Mkuu wa Shirikisho hilo Bw. Cai Guanshen ameeleza kuwa, Hongkong imekuwa ni mlango wa mawasiliano kati ya China Bara na nchi za nje katika ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kuonesha umuhimu mkubwa. Anasema:

    "Hongkong ikiwa jiji kubwa la kimataifa, imekuwa ikichukuliwa kama ni mlango muhimu wa mawasiliano kati ya China Bara na nchi za nje. Pia ni mfanya mawasiliano, mshiriki na mjenzi katika kuhimiza ushirikiano wa 'Ukanda mmoja, Njia moja'. "

    Bw. Cai amesisitiza kuwa ingawa hali isiyoweza kutabirika duniani, na matukio yaliyotokea hivi karibuni mkoani Hongkong zimeleta changamoto kwa maendeleo ya Hongkong, lakini anaamini kuwa Hongkong hakika itaondokana na matatizo yanayoikabili, na kuendelea kuonesha sifa yake kuchangia kukidhi mahitaji ya nchi.

    Mkurugenzi wa Idara ya biashara na ukuaji wa uchumi ya Hongkong Bw. Qiu Tenghua, ameeleza kuwa pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" limeifanya Hongkong itambue tena sifa yake, na kuhudumia vizuri zaidi nchi. Anaamini kuwa Mkutano wa nne wa Baraza la kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" unaoendelea mkoani Hongkong utaifanya Hongkong ioneshe umuhimu zaidi katika ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kuleta thamani kubwa zaidi. Anasema:

    "Huu ni mwaka wa nne wa kuhimiza maendeleo ya baraza hilo, na idadi ya washiriki imefikia 5,288, ambao ni wengi zaidi kuliko mwaka jana."

    Washiriki wanaona Hongkong ikiwa kituo cha fedha cha kimataifa, na soko kubwa zaidi la fedha za RMB Offshore RMB market, inaweza kutoa misaada katika kukusanya na kusimamia fedha kwa ajili ya miradi ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako