• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanya biashara Tanzania watakiwa kuridhia mkataba wa AFCFTA

    (GMT+08:00) 2019-09-13 19:59:18

    Wafanyabiashara nchini Tanzania wamesema Serikali haina budi kuridhia mkataba wa soko huru la Afrika (AfCFTA) pamoja na kufanya kampeni maalumu ya kuwaelewesha Watanzania juu ya fursa wanazoweza kuzipata kupitia mkataba huo.

    Taasisi ya Sekta binafsi Tanzania (TPSF) iliandaa mkutano na wafanyabiashara kujadili mustakabali wa Tanzania kuelekea AfCFTA na namna Tanzania inavyopaswa kujiandaa na soko hilo ambapo kwa pamoja wafanyabiashara waliohudhuria wamesema soko lina fursa nyingi kuliko hasara.

    Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya Infotech investment Group, Ali Mfuruki amesema Tanzania haina budi kuridhia mkataba huo bila hofu kwani kuna nchi kubwa na ndogo ambazo tayari zimeridhia na nyingine zinaendelea.

    Mwaka jana Tanzania na nchi nyingine 44 za Afrika zilisaini mkataba huo lakini nchi chache ziliridhia. Mfuruku amesema ni muhimu kuridhia na kujiandaa kwani bila kujiandaa mkataba huu utazinufaisha nchi zilizo tayari tu na Watanzania wafahamu kuwa biashara ni kuvuka mipaka na mkataba huu unaleta urahisi wa kuvuka mipata.

    Mufuruki amesema Afrika inaweza kuendelea kwa kufanya ushirika ili sehemu kubwa ya biashara katika bara hili ibaki Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako