• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afueni kwa raia, pigo kwa wabunge Rais kukataa kutia saini mswada wa PSC

    (GMT+08:00) 2019-09-13 19:59:35
    Walipa kodi nchini Kenya wamepata afueni kubwa baada ya Rais Uhuru Kenyatta kukataa kusaini mswada ambao ungewapa wabunge uwezo wa kujipatia marupurupu ya juu.

    Wabunge walikuwa wamepenyeza kipengee katika Mswada wa Tume ya Huduma za Bunge (PSC) wa 2018 na hivyo kuipa uwezo tume hiyo kuwaongezea marupurupu ya usafiri humu nchini na katika mataifa ya nje bila kuhusisha Tume ya Kukadiria Mishahara na Marupurupu ya Watumishi wa Umma (SRC).

    Mswada huo pia uliipa PSC mamlaka ya kukadiria kiwango cha marupurupu ambacho wabunge na maseneta wangekuwa wakipokea wanaposafiri nje ya Nairobi kwa shughuli zinazohusiana na majukumu yao.

    Rais Kenyatta alirejesha mswada huo katika bunge huku akiuandamanisha na memoranda kuhusu sehemu ambazo zinapafaa kufanyiwa mabadiliko. Wabunge sasa wana kibarua kigumu cha kubatilisha mapendekezo kwenye memoranda ya Rais kwani wanahitaji kufanya hivyo kupitia upigaji kura wa angalau thuluthi mbili ya wabunge wote. Hii ni sawa na wabunge 233 kati ya 349.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako