• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaongeza baadhi ya bidhaa za kilimo za Marekani kwenye orodha ya bidhaa zisizoongezwa ushuru

    (GMT+08:00) 2019-09-13 20:02:04

    Kamati ya ushuru wa forodha ya Baraza la Serikali la China imesema itaweka baadhi ya bidhaa za kilimo za Marekani kama vile maharage ya soya na nyama ya nguruwe kwenye orodha ya bidhaa zisizoongezwa ushuru.

    Habari kutoka Kamati ya Taifa ya Maendeleo na Mageuzi na Wizara ya Biashara ya China, zinasema China inayaunga mkono makampuni yanayonunua kiasi fulani cha mazao ya kilimo kuendana na kanuni za soko na za Shirika la biashara duniani WTO

    Hatua ya China imekuja baada ya Marekani kuamua kufanya marekebisho kwenye orodha ya bidhaa za China ziatakzotozwa ushuru kuanzia Oktoba Mosi.

    China ina soko kubwa na ina uwekezano mkubwa wa kuagiza bidhaa za kilimo zenye ubora wa juu kutoka Marekani. China inatumai kuwa Marekani itatekeleza ahadi yake na kuweka mazingira mazuri ya ushirikiano mzuri kwenye sekta ya kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako