• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kundi la Houthi la Yemen lasema miundombinu ya mafuta ya Saudi Arabia iliyoshambuliwa bado ni shabaha ya mashambulizi

  (GMT+08:00) 2019-09-17 08:18:06

  Kundi la Houthi la Yemen jana lilisema, miundombinu ya mafuta nchini Saudi Arabia iliyoshambuliwa bado ni shabaha ya mashambulizi ya kundi hilo.

  Kundi hilo limebainisha kuwa, maeneo mawili waliyoshambulia hivi karibuni huenda yakashambuliwa tena wakati wowote, pia limezionya kampuni zilizoko kwenye maeneo hayo na wageni kuondoka. Vilevile limeitaka Saudi Arabia isitishe uvamizi na vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Yemen.

  Awali jeshi la muungano linaloongozwa na Saudi Arabia lilisema, uchunguzi unaonesha kuwa silaha zilizotumika kwenye mashambulizi dhidi ya Shirika la mafuta la Saudi Arabia zinatoka Iran. Msemaji wa jeshi hilo amesema jeshi la muungano linafanya uchunguzi kuhusu mahali silaha ziliporushwa, na litatangaza matokeo kwa vyombo vya habari baada ya uchunguzi kumalizika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako