• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda na Uganda zasisitiza tena ahadi ya kujizuia kufanya vitendo vya uhasama dhidi ya upande mwingine

    (GMT+08:00) 2019-09-17 09:11:15

    Rwanda na Uganda zimesisitiza tena ahadi yao ya kujizuia kufanya vitendo vyovyote vya uhasama dhidi ya upande mwingine kufuatia mkutano wa kwanza wa kamati maalumu ya makubaliano yaliyosainiwa mwezi wa Agosti ya kusimamisha uhasama kati ya nchi hizo mbili.

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame walisaini makubaliano hayo katika mkutano wa pande nne ambao pia ulihudhuriwa na rais Joao Lourenco wa Angola aliyeongoza mkutano huo na rais Felix Tshisekedi wa DRC huko Luanda.

    Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano huo uliofanyika huko Kigali, Rwanda imetoa orodha ya wananchi wake waliozuiwa nchini Uganda na Uganda imeahidi kuthibitisha taarifa hizo kwa ajili ya kushughulikia majina hayo kupitia mchakato wa kisheria na kuwaachia wale ambao hawajakutwa na ushahidi wa kutenda uhalifu. Pia nchi hizo mbili zimekubaliana kukamilisha makubaliano ili kutoa mwongozo wa kubadilishana wahalifu wa jinai katika siku za baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako