• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Marubani wa Kenya Airways (KQ) watishia kugoma

  (GMT+08:00) 2019-09-17 19:54:27

  Marubani wa shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways (KQ) wataamua kesho watafanya mgomo baada ya ilani ya siku saba ya kuwacha kuwaajiri marubani kwa mkataba kuisha.

  Alhamisi iliyopita, Katibu Mkuu wa Chama cha Marubani wa Kenya (Kalpa) Murithi Nyaga aliandika barua kwa shirika hilo akitaka kusimamishwa kuajiri marubani 20 wa mkataba, akisema ni kinyume cha sheria.

  Wiki iliyopita, Mkurugenzi Mtendaji wa KQ anayemaliza muda wake Sebastian Mikosz, alitangaza kuajiri marubani 20 kwa mkataba kwa ndege zake aina ya Boeing 737.

  Marubani wanashutumu shirika hilo kwa kutotii makubaliano ya pamoja .

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako