• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Afrika kupambana na upoteaji wa chakula baada ya mavuno barani Afrika

  (GMT+08:00) 2019-09-18 09:55:01

  Umoja wa Afrika jana ulieleza juhudi zake kubwa za kupambana na upoteaji wa chakula baada ya mavuno barani Afrika ambacho kinaweza kulisha makumi ya mamilioni ya watu barani humo.

  Upoteaji wa chakula duniani unakadiriwa kufikia tani bilioni 1.3, kikiwa ni sawa na zaidi ya asilimia 30 ya chakula chote kinachozalishwa kwa matumizi ya wanadamu, na kile kinachopotea kinaweza kulisha watu takriban bilioni 1.6 kila mwaka.

  Barani Afrika, upoteaji wa chakula unakadiriwa kufikia tani 100. Mkurugenzi wa Kitengo cha Uchumi Vijijini cha Tume ya Uchumi na Kilimo Vijijini ya Umoja wa Afrika Janet Edeme, amesema thamani ya upoteaji wa nafaka pekee baada ya mavuno ni sawa na dola za kimarekani bilioni 4 kwa mwaka, ambacho kinaweza kukidhi mahitaji ya chakula ya watu milioni 48.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako