• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Afrika uko tayari kushirikiana kwa nguvu na China kukabiliana na changamoto baada ya mavuno barani Afrika

  (GMT+08:00) 2019-09-18 19:35:06

  Umoja wa Afrika umeonesha utayari wa kuhimiza ushirikiano na China kwenye kushughulikia changamoto baada ya mavuno barani Afrika.

  Mkuu wa idara ya uchumi wa vijijini wa Kamati ya uchumi wa vijijini na kilimo ya Umoja wa Afrika Bibi Janet Edeme, amesema hayo kwenye mkutano na wanahabari kuhusu Mkutano wa pili wa Baraza kuhusu hali baada ya mavuno barani Afrika unaoendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Addis Ababa.

  Amesema Umoja wa Afrika unatarajia kuimarisha ushirikiano na China kwenye kupunguza hasara inayotokea baada ya mavuno. Amekumbusha kuwa hivi karibuni Umoja wa Afrika na China walisaini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano kwenye usalama wa chakula na ubora, na usimamizi wa hasara baada ya mavuno, na kusema Afrika inatarajia kutumia teknolojia za China kukabiliana na changamoto hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako