• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Biashara kati ya Tanzania na Uganda bado haijapiga hatua

  (GMT+08:00) 2019-09-18 19:43:21

  Wizara ya bishara ya Uganda imesema Biashara kati ya Uganda na Tanzania haijawahi kuwa na usawa au kufanya vyema licha ya mipango kadhaa ya kuiboresha kati ya nchi hizo mbili .

  Licha ya kuwa nchi zote mbili ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), waagizaji wa Uganda, wamekuwa wakikabiliwa na vizuizi kwenye soko la Tanzania.

  Kulingana na takwimu za wizara ya biashara, biashara ya Uganda na Kenya na nchi zingine wanachama wa EAC inakua kwa kasi, lakini hali ni tofauti kati yake na Tanzania.

  Ripoti ya utendaji wa sekta ya biashara ya kila mwaka ya Wizara hiyo, inaonyesha kuwa Uganda kwa mara ya kwanza katika miongo kadhaa, ilisajili usawa wa biashara na Kenya katika mwaka wa fedha 2017/18 wa dola milioni 122.78 milion, lakini kulikuwa na nakisi kwa upande wa Tanzania.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako