• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujumbe wa China mjini Geneva wafanya kongamano kuhusu mafanikio ya maendeleo ya shughuli za haki za binadamu mkoani Xinjiang

    (GMT+08:00) 2019-09-19 09:30:29

    Ujumbe wa China katika ofisi za Umoja wa Mataifa na mashirika mengi ya kimataifa mjini Geneva jana Jumatano ulifanya kongamano kuhusu "mafanikio ya maendeleo ya shughuli za haki za binadamu mkoani Xinjiang", ambapo mabalozi wa nchi mbalimbali waliotembelea Xinjiang hivi karibuni na wataalamu wa haki za binadamu wa China wamealikwa kutoa maoni yao kuhusu hali ya mkoani humo.

    Kiongozi wa ujumbe huo Bw. Chen Xu akihutubia katika ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika kando ya Kikao cha 42 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, amesema mkoa wa Xinjiang umefanikiwa kuzuia mwelekeo wa kuongezeka kwa matukio ya kigaidi baada ya kuchukua hatua madhubuti za kupambana na ugaidi na itikadi kali ikiwemo kujenga vituo vya elimu na mafunzo ya ufundi stadi, na haukushuhudia tukio hata moja la kigaidi katika miaka mitatu iliyopita. Ameongeza kuwa mafanikio hayo yaliyopatikana mkoani Xinjiang yametoa uzoefu kwa jumuiya ya kimataifa katika kupambana na ugaidi na kuondoa itikadi kali, na China inapenda kubadilishana uzoefu huo na pande mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako