• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki Kuu ya Rwanda kuzindua kampeni ya tatu ya mfumo wa malipo ya kielektroniki

    (GMT+08:00) 2019-09-19 19:28:11
    Benki Kuu ya Rwanda mwezi ujao itazindua kampeni yake ya tatu ya mfumo wa malipo ya kielektroniki ili kuongeza matumizi ya malipo ya kielektroniki.

    Hii inaenda sambamba na malengo ya serikali ya kuwa na uchumi usiotumia pesa taslimu.

    Hii itakuwa kampeni ya tatu kufanya na Benki Kuu ya Rwanda na wadau kupiga jeki juhudi za uchumi usiotumia pesa taslimu tangu mwaka 2015.

    Kulingana na Takwimu za Benki ya Kitaifa ya Rwanda,idadi ya miamala ambayo ilifanywa kupitia vituo vya uuzaji iliongezeka hadi milioni 2.2 kufikia Juni mwaka huu kutoka milioni 1.5 mwezi Juni mwaka jana.

    Thamani ya miamala kupitia vituo vya uuzaji katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2019 ilikuwa Rwf100 bilioni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako