• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa biashara kati ya Ethiopia na Tunisia wafanyika Addis Ababa

    (GMT+08:00) 2019-09-19 19:28:28
    Mkutano wa kibiashara kati ya Ethiopia na Tunisia ulifanyika jana jijini Addis Ababa Ethiopia.

    Wawekezaji zaidi ya hamsini kutoka Tunisia na wanachama wa jamii ya wafanyabiashara nchini Ethiopia walishiriki katika mkutano huo.

    Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia,Markos Tekle katika mkutano huo jana,alisema mkutano huo unachukua jukumu kubwa katika kuimarisha mahusiano ya biashara na uwekezaji kati ya Ethiopia na Tunisia.

    Aidha alitoa wito kwa wawekezaji kutoka Tunisia kuwekeza nchini Ethiopia.

    Kwa upande wake,Waziri wa mambo ya nje wa Tunisia,Hatem Ferjani,alisema nchi hizo mbili ziko tayari kuendelea kuimarisha mahusiano yao katika biashara na uwekezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako