• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-NBC yashirikiana na Shirika la Posta

    (GMT+08:00) 2019-09-19 19:28:45
    Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya uwakala wa huduma za kibenki na Shirika la Posta nchini Tanzania,ili kupanua wigo wa huduma za benki hiyo sambamba na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha hasa maeneo ya vijijini.

    Hatua hiyo inatajwa kuwa itaongeza wigo wa mtandao wa utoaji huduma za kifedha kwa njia ya kidijitali,huku ikienda sambamba na azma ya serikali ya kupanua ushiriki wa wananchi katika shughuli za kifedha.

    Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa kutoa huduma za benki kati ya posta na NBC jijini Dar es Salaam jana,Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano ,Mhandisi Isaac Kamwelwe,alisema kupitia mtandao wa ofisi za Shirika la Posta nchini Tanzania lenye mtandao wa matawi 370,kutaiwezesha Benki ya NBC kuwafikia maelfu ya wananchi nchi nzima katika utoaji wa huduma zake za kibenki kwa gharama nafuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako