• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • NBC yafanya makubaliano na Posta Tanzania kuhusu huduma za fedha

    (GMT+08:00) 2019-09-20 20:00:38

    Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya uwakala wa huduma za kibenki na Shirika la Posta Tanzania ili kupanua wigo sambamba na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha hasa maeneo ya vijijini.

    Hatua hiyo inatajwa kuwa itaongeza wigo wa mtandao wa utoaji huduma za kifedha kwa njia ya kidijitali huku ikienda sambamba na azma ya serikali ya kupanua ushiriki wa wananchi katika shughuli za kifedha (financial inclusion).

    Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania Bw Isack Kamwelwe amesema kupitia mtandao wa ofisi za Shirika la Posta lenye matawi 370, kutaiwezesha NBC kuwafikia maelfu ya wananchi nchi nzima katika utoaji wa huduma zake kwa gharama nafuu.

    Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi amesema ushirikiano huo utawawezesha kutumia mifumo ya kidijitali na wingi wa ofisi za posta katika kutoa huduma za kibenki nchi nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako