• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • LANGALANGA: Vettel alimaliza ukame wa muda mrefu kwa kushinda katika Singapore Grand Prix

  (GMT+08:00) 2019-09-23 09:57:41

  Sebastian Vettel wa Ferrari jana alimaliza ukame wa mwaka mzima kwa kushinda katika mashindano ya langalanga ya Singapore Grand Prix baada vya kuonesha ufundi wa aina yake wa kukamata usukani na kuweka rikodi ya ushindi wa tano kwenye mashindano hayo. Mjerumani huyo alikuwa akikimbizwa na dereva wa timu yake Charles Leclerc, aliyeanza vizuri lakini baadaye akapoteza uongozi kwa bingwa huyo mara nne wa dunia baada ya kusimama kidogo kuongeza mafuta na kuifanyia sevisi gari yake, na Max Verstappen wa Red Bull, akamaliza nafasi ya tatu. Bingwa kiongozi Lewis Hamilton amemaliza wa nne lakini alimpa nafasi nzuri dereva wa timu yake ya Mercedes Valtteri Bottas ya pointi 65 akiwa amesaliwa na mbio sita, baada ya Mfinland huyo kumaliza nafasi ya tano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako