• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Maendeleo ya Afrika iliidhinisha pendekezo la dola milioni 17,7 kwa mradi wa kwanza wa elimu

    (GMT+08:00) 2019-09-23 18:39:26
    Bodi ya Benki ya Maendeleo ya Afrika iliidhinisha pendekezo la dola milioni 17,7 mnamo mwezi septemba ili kufadhili mradi wa kwanza wa sekta ya kijamii huko Sudani Kusini.

    Mradi huo utaboresha elimu ya msingi kwa watoto.

    Mradi huo utaboresha upatikanaji wa elimu ya msingi kwa watoto 30,000 kupitia ukarabati na upanuzi wa shule 35 za msingi, hivyo kuongeza uwezo wa walimu 2000 na kukarabati vituo viwili vya kitaifa vya mafunzo ya ualimu na vituo kumi vya elimu.

    Mradi huo unaongozwa na mkakati wa kitaifa wa maendeleo ya Sudani Kusini, Mkakati wa jumla wa elimu. Mikakati hiyo inasisitiza kujenga taifa kupitia uwezo na maendeleo ya miundombinu.

    Mgogoro Sudani Kusini umeathiri vibaya maendeleo ya kiuchumi na miundombinu ya huduma za kimsingi ikijumuisha elimu huko Sudani Kusini.

    Zaidi ya watoto milioni 2.2 nchini Sudani Kusini hawaendi shuleni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako