• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya Saruji ya Portland imefuta kazi mameneja wote kupunguza gharama

    (GMT+08:00) 2019-09-23 18:40:52
    Kampuni ya Saruji ya Portland East Africa (EAPCC) imefuta kazi mameneja wote wa juu huku kukiwa na mpango wakuuza ekari 2000 ya ardhi yake huko Mavoko, Machakos, kuongeza fedha zake.

    Kampuni hiyo wiki iliyopita ilipeana barua za kusimamishwa kazi kwa wasimamizi na mameneja 136.

    Portland ilipata hasara ya jumla ya Sh bilioni 1.26 katika miezi sita hadi Desemba, ikilinganishwa na upotezaji wa Sh milioni 966 katika kipindi kama hicho mwaka uliopita.

    Wafanyikazi wadogo watafutwa kazi wakati kiwanda hicho kitauza ardhi ya ekari 2000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako