• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mafanikio ya China katika kupunguza umaskini yametoa uzoefu wenye thamani kwa Ghana

  (GMT+08:00) 2019-09-23 19:46:45

  Uzoefu wa China katika juhudi za kupambana na umaskini nchini China uliopatikana kwa miaka kadhaa, umetoa funzo muhimu kwa Ghana katika kupambana na umaskini.

  Ofisa wa mamlaka ya maendeleo Kaskazini mwa Ghana Bw. George Kwabena ambaye amemaliza ziara yake katika maeneo ya kusini magharibi mwa China yaliyoathirwa na umaskini, amesema amefurahishwa sana na mabadiliko ya kasi ambayo watu wa maeneo ya kusini mwa China wameyaona kutokana na juhudi za serikali.

  Amepongeza uvumbuzi wa China katika kupunguza umaskini kama ni kichocheo cha kuendeleza jamii za vijijini. Amesema China na Ghana zina mitazamo sawa kwenye kupunguza umaskini, na Ghana inasumbuliwa na matatizo kadhaa kama vile miundo mbinu mibaya na kukosekana kwa uwekezaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako