• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: NBC yazindua mkopo wa bima

    (GMT+08:00) 2019-09-24 16:55:40
    Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua mkopo wa bima unaoanzia Sh1 milioni ukiwalenga zaidi wafanyabiashara walio katika sekta ya uchukuzi.

    Akizungumza na washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (Tatoa) jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru amesema mkopo huo utaanzia Sh1 milioni hadi Sh300 milioni.

    Amesema mkopo wa bima wa NBC ni maalumu kwa ajili ya bima za biashara zote zikiwemo magari, bidhaa zilizo safarini, majanga ya moto, ujambazi, hatari za barabarani na ajali kwa wafanyakazi.

    Mkurugenzi huyo amesema uamuzi wa kuanzisha huduma hiyo inayowalenga wafanyabiashara umetokana na kasi ya utendaji wa serikali ikiwemo kuondoa kero zilizokuwa zikiizorotesha sekta ya uchukuzi nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako