• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wawekezaji wa Marekani watakiwa kuifanya Kenya kuwa chaguo lao

    (GMT+08:00) 2019-09-25 19:05:41

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amewataka wawekezaji wa Marekani kuifanya Kenya kuwa chaguo lao barani Afrika.

    Rais alisema Nguzo Nne za Ajenda Kuu ya Maendeleo ya Serikali yake, hususan uzalishaji ambapo Serikali inapanga kuinua mchango wa sekta hiyo kwenye uchumi kutoka asilimia 8.4 ya sasa ya Pato la Kitaifa hadi asilimia 15 ifikapo mwaka 2022, inatoa nafasi nyingi kwa kampuni za Kimarekani.

    Rais Kenyatta aliyasema hayo alipokuwa akihutubia kongamano la sekta ya kibinafsi lililoandaliwa na Shirika la Biashara nchini Marekani na kuhudhuriwa na maafisa wakuu wa kampuni kubwa za kimataifa kutoka Marekani. Uhuru amesema Kenya inatafuta ushirikiano wa kudumu wa kibiashara na mashirika ya Marekani.

    Kando na uzalishaji, Rais alisema kujitosheleza kwa chakula na lishe bora, makaazi nafuu na Afya Bora kwa Wote ni sekta zingine ambazo zina uwezo mkubwa wa uwekezaji.

    Rais Kenyatta alisema lengo la Serikali yake la kujenga nyumba 500,000 za gharama nafuu lingalipo na akazirai kampuni za Marekani kutenga rasilimali kwa mpango huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako