• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watafiti wakutana kutathmini maendeleo ya kilimo

    (GMT+08:00) 2019-09-25 19:06:13

    Watafiti 110 wa mazao na mifugo kutoka katika mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na halmashauri zake, wameshiriki mkutano wa tathmini ya utekelezaji wa mapendekezo ya kilimo ya mwaka wa fedha 2018/19 katika ukanda huo.

    Mkutano huo ulifanyika kwa siku mbili katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari) Kituo cha Uyole, jijini Mbeya na taasisi hiyo iliwajulisha kuwa imeandaa aina 55 za mbegu mpya za mazao mbalimbali ambazo zinaendana na uchumi wa viwanda.

    Mkurugenzi wa Tari- Uyole, Dk. Tulole Bucheyeki, alisema lengo la mkutano huo ilikuwa kuangalia changamoto zilizowakabili wakulima katika msimu uliopita na kujadili namna ya kuzitatua ili zisikwamishe juhudi za uzalishaji msimu mpya unaokuja.

    Alisema pia mkutano huo ulilenga kutambulisha mbegu mpya za mazao zilizofanyiwa utafiti ili wataalamu hao wakazisambaze kwa wananchi na kwamba mbegu hizo zina manufaa makubwa kutokana na uzaaji wake.

    Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, wanataka kumwondoa mkulima wa mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwenye kilimo cha mazoea na kumfanya azalishe kibiashara ili anufaike zaidi na shughuli hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako