• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China ndio nchi yenye mipango mikubwa ya uwekezaji Uganda

    (GMT+08:00) 2019-09-25 19:06:33

    China imeandikisha rekodi ya kuwa nchi yenye mipango mikubwa zaidi ya uwekezaji nchini Uganda katika mwaka wa 2018/2019 huku thamani ya uwekezaji wake ikiwa dola za kimarekani milioni 607.3 ikiwa ni asilimia 45.1 ya uwekezaji wote waliopanga. Wawekezaji wa Uganda walikuwa wa pili huku thamani yao ya uwekezaji ikiwa jumla ya dola za kimarekani milioni 328.7 huku ikifuatiwa kwa karibu na nchi za Lebanon, India na Milki za kiarabu. Idadi ya wawekezaji wa China wanaoonyesha nia ya kuwekeza nchini humo imeongezeka ambapo wengi wao wamejikita katika utengenezaji bidhaa na ujenzi. Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya uwekezaji nchini Uganda Bwana Lawrence Buyesi amesema tayari wametoa leseni kwa miradi mipya ya uwekezaji 286 katika mwaka wa 2018/2019 yenye thamani ya shilingi bilioni 1.34 na yenye uwezo wa kuunda ajira karibu elfu 60. Katika kipindi cha mwaka wa 2017 China alikuwa mshirika wa pili wa kibiashara na Uganda huku thamani yake ikiwa dola za kimarekani milioni 850. Kuna jumla ya makampuni 200 ya wachina nchini Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako