• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mradi wa "Two mountains lodge Ltd" wasaidia wananchi mil. 13

    (GMT+08:00) 2019-09-25 19:06:59

    Mradi wa 'Two mountains lodge Ltd'nchini Tanzania umetoa msaada wa Sh. milioni 13.5, kuchangia miradi mbalimbali ya huduma za kijamii na maendeleo kwa wakazi wa Kijiji cha Ngorika, Kata ya Nkoaranga wilayani Arumeru, ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuwaletea wananchi maendeleo na kufikia uchumi wa kati. Akizungumza na wanahabari, mshauri wa mradi huo, Laisser ole Mattasia, alisema kampuni hiyo ilitoa mchango huo kuanzia mwaka 2014 ulipoanza kutekelezwa hadi 2019 kwa nyakati tofauti.

    Alisema mradi huo umegharimu Sh. bilioni 3.5 hadi kukamilika, kwa hatua ya kutoa huduma, ulitumia Sh. milioni 1.5 kujenga kisima cha kuhifadhia maji, kwenye eneo la Lodge ambalo wanakijiji cha Ngorika hupata huduma ya majiAlisema kwa sasa wakulima wanasafirisha mazao yao kama mboga na ndizi kwa urahisi kupeleka sokoni.

    Hata hivyo, wameiomba serikali kuiboresha kwa kiwango cha changarawe na hata lami.

    Alisema mradi huo umechangia Sh. milioni mbili kwa ajili ya ukarabati wa chumba cha kuhifadhia maiti kwenye Hospitali ya Nkoaranga, eneo lililopo karibu na mradi huo na kuwasaidia wakazi kuondokana na gharama za usafiri kupeleka miili ya ndugu zao katika Hospitali ya Mount Meru.

    Ole Mattasia, alisema mradi huo wenye vyumba 34 vya kulaza wageni, umetekelezwa na kugharamiwa na Watanzania wazawa toka wilayani hapo akiwamo Dk. Ndosi, ambaye alishastaafu kazi nchini na kwenda kufanya kazi nchini Botwsana.

    Alisema mradi huo umetoa ajira za kudumu kwa wazawa 17.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako