• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yalinda kithabiti mfumo wa pande nyingi

    (GMT+08:00) 2019-09-25 19:47:50

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres kwenye mjadala wa kawaida wa mkutano wa baraza kuu la 74 la Umoja wa Mataifa amezihimiza nchi wanachama kudumisha dunia yenye ncha nyingi.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China siku zote inalinda kithabiti lengo na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa na kulinda mfumo wa pande nyingi. Bw. Guterres amezihimiza nchi 193 wanachama kufanya juhudi kuepusha hali ya kutengana, na kudumisha mfumo wa dunia katika sekta mbalimbali ukiwemo uchumi na sheria ya kimataifa, na nchi zenye ncha nyingi na mashirika makubwa ya pande nyingi.

    Bw. Geng amesema China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali duniani kuhimiza kujenga uhusiano mpya wa kimataifa wa kuheshimiana na kunufaishana wenye usawa na haki na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako