• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China ahudhuria mkutano kuhusu suala la nyuklia la Iran

    (GMT+08:00) 2019-09-26 09:19:39

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana huko New York amehudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kuhusu suala la nyuklia la Iran.

    Bw. Wang Yi amesema, Marekani kutoa shinikizo kubwa dhidi ya Iran ni chanzo cha kimsingi cha msukosuko wa suala la nyuklia la Iran. Kama hali hiyo itazidi kuwa mbaya, itasababisha msukosuko mkubwa zaidi, na kuzitaka pande mbalimbali zifanye juhudi kuhimiza suala la nyuklia la Iran litatuliwe kwa njia ya kisiasa na kidiplomasia.

    Amesema China ina mapendekezo manne kuhusu suala hilo, ikiwemo kushikilia kanuni ya kimsingi ya kulinda utaratibu wa pande nyingi, kushikilia kutekeleza ahadi ya makubaliano, kushikilia njia sahihi ya kutatua migongano kwa njia ya mazungumzo, na kushikilia mwelekeo wa kuhimiza amani ya kikanda.

    Bw. Wang Yi pia amehudhuria mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na mashirika ya kikanda kuhusu ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako