• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RAGA: Wanaraga wa Morans wa Kenya kujipima nguvu kwa kucheza na timu mbalimbali za kimataifa

    (GMT+08:00) 2019-09-26 10:00:06

    Kikosi cha Kenya cha raga ya daraja la pili kwa wachezaji saba kila upande almaarufu Morans kimepangiwa kushiriki michuano mbalimbali ya vipute visivyo rasmi msimu ujao. Haya ni kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Shirikisho la Raga la Kenya (KRU), Oduor Gangla ambaye amekariri kwamba vipute hivyo vitatoa jukwaa mwafaka kwa wanaraga wa Kenya kujipima nguvu kadri wanavyojiandaa kwa mapambano mbalimbali ya haiba kubwa yaliyopo mbele yao. Kati ya vipute ambavyo Morans wanatazamiwa kushiriki ni Dubai Invitational, Roma Sevens, Singapore Invitational a Sudamerica Sevens kitakachoandaliwa nchini Argentina.

    Gangla anasema kuwa inasikitisha kwamba kivumbi cha pekee ambacho wanaraga wa Morans hushiriki kwa sasa ni cha Safari Sevens ambacho kwa mujibu wake, hakitoshi kabisa kuwapa ujuzi wa kukabiliana na wapinzani walio na tajriba pevu na uwezo mkubwa katika raga ya kimataifa kila wanapojumuishwa katika kikosi cha Shujaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako