• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Rais wa Bayern Munich atishia kuwazuia wachezaji wa klabu yake kuchezea timu ya taifa

    (GMT+08:00) 2019-09-26 10:00:25

    Rais wa Bayern Munich, Uli Hoeness ametishia kuwazuia wachezaji wa klabu hiyo kuchezea timu ya taifa kama Manuel Neuer atapoteza nafasi yake ya kuwa kipa wa kwanza wa Ujerumani. Kipa wa Barcelona, Marc-Andre Ter Stegen, mwenye miaka 27, kwa sasa ni kipa wa pili wa Neuer na ameeleza kutofurahishwa kwa kuwekwa benchi katika timu ya taifa na kipa huyo mzoefu wa Bayern Munich. Wachezaji hao wawili wametupiana maneno na wiki iliyopita Ter Stegen alimtuhumu Neuer kwa kusema "maneno ambayo si sahihi". Hoeness, hata hivyo, amezungumza kwa niaba ya Neuer na kumkosoa kocha wa Ujerumani, Joachim Low na Shirikisho la Soka la Ujerumani kwa kutowalinda wachezaji nyota wa Bayern kwa kusema hawatakubali kufanywa mabadiliko na kusisitiza kuwa kabla ya kutokea hilo watawazuia wachezaji wao wote kujiunga na timu ya taifa. Low aliahidi kumpa Ter Stegen muda zaidi wa kucheza mwaka 2019 lakini hadi sasa amecheza mechi moja tu, akicheza kwa dakika 45 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Serbia mwezi Machi. Chini ya sheria za FIFA, Bayern inaweza kukabiliwa na adhabu ya kuanzia kutozwa faini hadi kuondolewa katika mashindano ya chama hicho cha soka barani Ulaya kwa kuzuia wachezaji wake kuchezea timu ya taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako