• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga Marekani kuyakandamiza makampuni ya China kwa kufuata sheria za ndani

    (GMT+08:00) 2019-09-26 19:20:21

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, China inapinga Marekani kuweka vikwazo dhidi ya makampuni na watu wa China, na siku zote inaipinga Marekani kuweka vikwazo vya upande mmoja na kuwa na "mamlaka ya mkono mrefu", kuyakandamiza makampuni ya China kwa kufuata sheria ya ndani.

    Bw. Geng amesema hayo kufuatia Marekani kutangaza kuweka vikwazo dhidi ya makampuni kadhaa na watu wa China. China imesisitiza kwa mara nyingi kuwa jumuiya ya kimataifa ikiwemo China inaanzisha ushirikiano na Iran chini ya utaratibu wa sheria za kimataifa, ambao unafuata sheria husika na kustahili kuheshimiwa na kulindwa. Marekani inapuuza maslahi halali za pande mbalimbali na kutumia ovyo vikwazo, na kukiuka vibaya kanuni za msingi za uhusiano wa kimataifa na kwenda kinyume na mwelekeo mkuu, na hatua hiyo haitatambuliwa na jumuiya ya kimataifa.

    Amesema China inaitaka Marekani irekebishe makosa yake. China imeanza na itaendelea kuchukua hatua za lazima ili kulinda kithabiti maslahi halali ya makampuni yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako