• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya Sukari ya Mumias yawekwa chini ya urasimu

    (GMT+08:00) 2019-09-26 19:43:53
    Kampuni ya sukari ya Mumias nchini Kenya imewekwa chini ya mrasimu.

    Hii ni baada ya Benki ya Kenya Commercial jumanne kumteua Meneja Mrasimu kusimamia shughuli za kampuni hiyo.

    Benki hiyo ilimteua Bw Ponangipalli Venkata Ramana Rao wa kampuni ya ushauri ya Tact Consultancy Services kusimamia shughuli za kampuni hiyo kubwa zaidi ya sukari nchini Kenya.

    Bw Rao alizuru kiwanda cha kampuni hiyo Jumanne na akawapa wasimamizi stakabadhi kuhusu shughuli za kampuni hiyo katika siku za hivi karibuni.

    Usimamizi wa kampuni hiyo umeshauriwa kuwasilisha taarifa kuhusu masuala ya kampuni hiyo kuanzia tarehe ya kuteuliwa kwa mrasimu.

    Vilevile, wasimamizi hao wanahitajika kuwasilisha orodha ya mali zote, ikiwemo magari yote na vifaa vinginevyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako