• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Wafugaji kunufaika na kiwanda cha mbolea

    (GMT+08:00) 2019-09-26 19:44:14
    Huenda wafugaji nchini Tanzania wakanufaika baada ya wawekezaji kuja na nia ya kuwekeza kwenye mifugo zikiwamo kwato,pembe,kinyesi,na manyoya ambazo zitakuwa zikinunuliwa kama malighafi nyingine ili kutumika kwenye kiwanda cha kutengenezea mbolea.

    Akizungumza jana ofisni kwake wakati akiwakaribisha wawekezaji kutoka Jamhuri ya watu wa Slovakia wa kampuni ya Rokosan inayojihusisha na utengenezaji wa mbolea kwa kutumia malighafi zitokanazo na mifugo Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Tanzania (mifugo),Profesa Elisante Ole Gabriel alisema lengo la serikali ni kuendelea kufungua milango kwa wawekezaji wote wenye nia ya kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali ikiwamo sekta ya mifugo nchini humo.

    Aidha miradi kama hii,alisema itasaidia kuhamasisha wananchi kuendelea kufuga kwa wingi na kwa tija baada ya kuona fursa za uwekezaji zikiongezeka.

    Ole Gabriel alisema wawekezaji walio tayari kuwekeza wanakaribishwa na Wizara inawaahidi ushirikiano wa hali ya juu kwenye sekta ya mifugo kwa jili ya kuinua hali za wafugaji nchini Tanzania ,kuongeza ajira,pia kuongeza ukusanyaji wa kodi kupitia bidhaa mbalimbali zikiwamo zitokanazo na viwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako