• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akutana na Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi

    (GMT+08:00) 2019-09-26 19:44:33
    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta jumanne alikutana na mwenzake wa Somalia Rais Mojhamed Abdullahi Mohamed katika mkutano uliopangwa na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi.

    Kenya na Somalia zimekuwa na mzozano kuhusu umiliki wa rasilimali ya mafuta na gesi katika mpaka wao ulioko bahari ya hindi.

    Kila moja inadai utajiri huo uko ndani ya nchi yake.

    Rais Kenyatta alikutana na kufanya mashauriano na Rais Mohamed jijini New York ambako kikao cha 74 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) kinaendelea.

    Aidha Rais Kenyatta pia alikutana na Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh.

    Wakati wa mikutano hiyo, viongozi hao walijadili masuala yanayohusu mataifa yao na bara la Afrika kwa jumla.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako