• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FIFA: Tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA yakumbwa na shutuma nzito

    (GMT+08:00) 2019-09-27 09:38:38

    Tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA imekumbwa na shutuma nzito juu ya kura zilizomchagua Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi kushinda tuzo hiyo ikidaiwa kura zilikuwa za uongo. Katika hatua nyingine Bodi inayoratibu tuzo hizo imesema kura za Nchi ya Misri ziliharibika hivyo kutohesabiwa kwasababu saini zilikuwa zimeandikwa kwa herufi kubwa. FIFA imeeleza hayo baada ya Chama cha Soka cha Misri kutaka kujua ni kwanini kura ya Kocha wa timu yao ya Taifa, Shawki Ghareeb na nahodha Ahmed hazikuhesabiwa. Aidha, Kocha wa timu ya Sudan, Zdravko Logarusic na nahodha wa Nicaragua, Juan Barrera wamedai kupitia Mitandao ya Kijamii kuwa kura zao zilizooneshwa na FIFA hadharani hazikuakisi machaguo yao. Lugorisic amedai kuwa chaguo lake la kwanza lilikuwa Mshambuliaji wa Misri, Mohammed Salah lakini FIFA imeonesha chaguo lake ni Messi huku Barrera naye akidai kutompigia kura Messi kama FIFA ilivyodai.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako