• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TENISI: Muaustralia Nick Kyrgios apigwa marufuku kwa wiki 16 na ATP kwa utovu wa nidhamu

    (GMT+08:00) 2019-09-27 09:39:13

    Nyota wa Tenisi kutoka Australia Nick Kyrgios jana alipokea adhabu ya kupigwa marufuku kwa wiki 16 na ATP na amewekwa kwenye uangalizi kwa miezi sita baada ya kuonesha tabia chafu na utovu wa nidhamu kwa kuongea kwa hasira na kufanya fujo uwanjani katika mwaka mmoja uliopita. Adahabu hiyo imeambatana na masharti yakiwemo kutafuta usaidizi wa mtaalamu anayeshughulikia tabia katika kipindi atakachokuwa akitumikia adhabu yake. ATP imesema adhabu ya marufuku itaondolewa baada ya miezi sita ya uangalizi kumalizika endapo atatimiza masharti aliyopewa. Mwezi uliopita aliwahi kupigwa faini ya dola za kimarekani 113,000 kwa matumizi mabaya ya mpira, kuondoka uwanjani bila ruhusa, kutumia lugha ya matusi na kuonesha dharau baada ya kushindwa na Mrussia Karen Khachanov katika michuano ya Cincinnati Masters.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako