• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • VOLIBOLI: Timu ya wanawake ya mpira wa wavu wa kuketi kufanya maandalizi kabambe Okinawa Japan

    (GMT+08:00) 2019-09-27 09:39:31

    Timu ya wanawake ya mpira wa wavu wa kuketi itakuwa na maandalizi kabambe kwa muda wa wiki mbili, mwezi Novemba katika uwanja wa Okinawa nchini Japan, kufuatia timu hiyo hivi karibuni kufuzu Michezo ya Walemavu itakayofanyika Tokyo Japan mwakani. Hata hivyo maandalizi hayo, zaidi yatakuwa kwa ajili ya uzinduzi wa Michezo ya Walemavu ya Afrika inayofanyika Januari 2020 huko Morocco. Ikiwa nchini Japan, timu hiyo pia itashiriki kwenye mashindano ya wanawake ya World Super 6 ambayo yanazikutanisha timu sita kati ya timu bora zaidi duniani za voliboli ya kuketi. Rwanda itaiwakilisha Afrika katika mashindano hayo ya wiki nzima ambayo yatakuwa November 12 hadi 17. Rwanda ilijikatia tiketi ya Michezo ya Walemavu ya Tokyo 2020 wiki iliyopita baada ya kuishinda Misri na kushikilia Ubingwa wa Afrika katika uwanja wa Amahoro.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako