• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TENISI:Andy Murray atolewa nje ya michuano ya Mabingwa ya Zhuhai

  (GMT+08:00) 2019-09-27 09:50:53

  Mchezaji Tenisi wa Uingereza Andy Murray ametolewa nje ya michuano ya Mabingwa ya Zhuhai ya China katika hatua ya 16 baada ya kushindwa na Muaustralia Alex de Minaur kwa seti 4-6 6-2 6-4. Mchezaji huyo aliyekuwa namba moja duniani sasa yupo nafasi ya 413 baada ya kufanyiwa upasuaji wa paja. Murray alikuwa na mategemo ya kuendeleza ushindi wake kama alioupata kwa Mmarekani Tennys Sandgren, ambao ni wa kwanza wa ATP Tour. Kama angefanikiwa kumshinda Alex de Minaur mchezaji aliyepo namba 31 duniani angejikatia tiketi ya robo fainali. Murray amesema alicheza kwa tabu na kiwango chake kimeshuka kidogo. Mwezi uliopita Murray mwenye miaka 32 alishinda lower-level Challenger Tour katika michuano ya wazi ya Rafa Nadal, lakini ushindi wa Jumanne wa seti tatu katika raundi ya kwanza ya Zhuhai Championships ulikuwa wa kwanza wa ATP Tour tangu Januari.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako