• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KRA yalaumiwa kwa kushindwa kukusanya Sh158 bilioni

    (GMT+08:00) 2019-09-27 18:25:26
    Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru Nchini Kenya (KRA) imelaumiwa kwa kushindwa kukusanya ushuru unaofikia kiasi cha Sh158 bilioni katika mwaka wa kifedha wa 2014/2015.

    Ufichuzi huo uko katika ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali ya mwaka huo ambayo ilikuwa ikikaguliwa na Kamati ya Bunge kuhusu Uwekezaji (PIC).

    Kamishna Mkuu wa KRA James Mburu ambaye alifika mbele ya kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir alisema kufikia sasa mamlaka hiyo imekusanya Sh112 milioni kati ya fedha hizo ambazo zimejilimbikiza kwa miaka minne.

    Bw Mburu aliwaambia wabunge hao kwamba KRA sasa imeweka mikakati murwa ya kuimarisha kiwango cha ukusanyaji ushuru mwingi.

    Bw Mburu aliwataja wafanyakazi kadha ambao wameshtakiwa kwa kukwepa kulipa mabilioni ya fedha kama ushuru, ishara ya kujitolea kwa KRA kukusanya ushuru zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako